Muhimbili: Hatuhusiki

HomeKitaifa

Muhimbili: Hatuhusiki

Hospitali ya Taifa Muhimbili imetoa taarifa ya kukataa kuhusika na usambazaji wa video inayomuonyesha Mwanamuziki Profesa Jay akiwa katika chumba cha wagonjwa walio chini ya uangalizi (ICU).

Video hiyo ilisambaa katika mitandao ya kijamii baada ya kuwekwa katika programu tumizi ya Mange Kimambi “Mange kimambi Software Application”.

Katika taarifa hospiatali ya Muhimbili imeeleza kuwa inahudumia wagonjwa takribani 3,400 ambao ni wananchi wa kawaida, wanasiasa na viongozi mbalimbali kwa kuzingatia taaluma, maadili na faragha za wateja wao.

Aidha wametoa pole kwa mke wa Profesa Jay, familia na wananchi wote walioguswa na tukio hilo, pia wakazitaka mamlaka husika kuingilia kati na kubaini chanzo cha video hizo na hatua stahiki zichukuliwe kwa aliyefanya kitendo hiko.

error: Content is protected !!