Mwalimu madrasa alawiti, mwanamke abaka mtoto

HomeKitaifa

Mwalimu madrasa alawiti, mwanamke abaka mtoto

Serikalini mkoani Arusha ikijipanga kumfikisha mahakamani mwalimu wa madrasa, Jumanne Ikungi anayetuhumiwa kuwalawiti wanafunzi 22 wa Shule ya Msingi Mkonoo, huko mkoani Iringa, Jeshi la Polisi linamshikilia Desderia Mbelwa kwa tuhuma za kumbaka mvulana wa miaka minne.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Said Mtanda alitoa maagizo ya wanafunzi kufanyiwa uchunguzi na madrasa kufungwa.

“Nimeagiza wanafunzi waendelee kufanyiwa uchunguzi katika hospitali na madrasa kufungwa hadi hapo uchunguzi utakapokamilika,” alisema.

Pia aliagiza wanafunzi wote kuandika kama wamefanyiwa matukio yoyote ya ukatili na baadaye Serikali itafanya uchunguzi.

Katika karatasi chache zilizokusanywa, baadhi ya wanafunzi walikiri kufanyiwa ukatili na mzee Jumanne anayeishi jirani na shule hiyo ambaye ndiyo mwalimu wa madrasa.

Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Allan Bukumbi  amesema tukio la Desderia (56) lilitokea Mei 8 katika kijiji cha Lumuli, Iringa vijijini.

Mwanamke huyo alimkamata kwa nguvu mtoto huyo wa miaka minne kisha kumbaka na kumsababishia maumivu makali sehemu za siri.

“Alimkata kwa nguvu mtoto huyo anayesoma darasa la tatu alipokuwa anatoka shuleni, akamvutia kichakani na kumtishia asiseme. Akafanya naye ngono, kitendo kilichomsababishia mtoto huyo maumivu makali na marejaha katika sehemu zake za siri,” alisema.

Desderia amekiri kutenda kosa hilo bila kutaja sababu za yeye kufanya hivyo na atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.

error: Content is protected !!