Mwanamke aliyemshtaki daktari wa mama yake kwa kuzaliwa ashinda kesi

HomeKimataifa

Mwanamke aliyemshtaki daktari wa mama yake kwa kuzaliwa ashinda kesi

Mwanamke ambaye alimshtaki daktari wa mama yake akidai kwamba hakupaswa kuzaliwa ameshinda kesi na kutakiwa kulipwa mamilioni ya fidia. Evie Toombes, mwana shoo nyota kutoka Uingereza, alifungua kesi ya kihistoria ya “mimba mbovu” dhidi ya daktari wa mama yake kwani alizaliwa na shida ya uti wa mgongo. 

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 20 alimpeleka Dkt Philip Mitchell kortini kwa kukosa kumshauri vyema mama yake alipokuwa mjamzito. Evie Toombes anadai kwamba ikiwa Dk Mitchell angemwambia mama yake alihitaji kuchukua virutubisho vya asidi ya folic ili kupunguza hatari ya ugonjwa wa mgongo kuathiri mtoto wake, angeahirisha kupata mimba. 

Jaji Rosalind Coe QC aliunga mkono kesi ya Evie katika uamuzi wa kihistoria wa Mahakama Kuu ya London na kusema kwamba ikiwa mama ya Evie angepewa ushauri sahihi uliopendekezwa, angechelewesha majaribio ya kushika mimba.

Mamake Evie Toombes alikuwa ameiambia mahakama hapo awali kwamba iwapo Dkt Mitchell alimshauri vyema, angeghairi mipango yake ya kupata ujauzito.

“Nilishauriwa kwamba ikiwa ningekuwa na lishe bora hapo awali, singelazimika kutumia asidi ya folic,” alimwambia Hakimu.

Uamuzi huo unachukuliwa kuwa wa msingi kwa sababu inamaanisha kuwa mtaalamu wa afya anaweza kuwajibishwa kwa ushauri usiofaa wa kabla ya kupata mimba iwapo itasababisha kuzaliwa kwa mtoto aliye na hali mbaya kiafya.

 

error: Content is protected !!