Japo kila mtu anakasoro zake, lakini kuna tabia ndogo ndogo ambazo huleta uharibifu kwenye mahusiano. Tabia hizo huondoa amani na furaha na kuleta uchungu.
Kwa kiasi kikubwa hayo hutokea pale mwanaume anapokosa umakini wakati wa uchaguzi wa mwenzi anayetaka kuwa naye.
Kuna aina za wanawake ambao mwanaume hapaswi kuwa nao kwenye mahusiano. Baadhi ya wanawake hao ni; w
- Mwanamke mwenye maneno machafu
Mwanamke anatakiwa awe na staha, sio kila neno linatoka mdomoni kwake. Muangalie akiwa na hasira anaongea nini lakini pia anaongea nini kuhusu watu ambao wako chini yake. Kama maneno yake hayaheshimu wengine, hata ukimuweka ndani hatakuheshimu. - Mwanamke mchoyo
Siku utakapoamua kuishi na mwanamke mchoyo hamtakuja kutembelewa na ndugu wala marafiki kwasababau ya uchoyo wa mke wako. Mwanamke mchoyo hawezi kutoa kitu chake kwa mtu kwani anajihisi kama anapoteza. - Mwanamke anayependa kwenda kwenye sherehe bila mpango.
Kuna wanawake wanapenda sana shughuli hata kama hana sababu ya kwenda kwenye shughuli hizo. Tabia hiyo inaweza kuwafanya watelekeze nyumba zao na majukumu yao ya msingi ili tu waende kwenye kila sherehe.
- Anaependa kupewa kipaumbele dhidi ya wengine katika namna isiyofaa
Japo ni jambo la kike kutaka kupewa kipaumbele na jamii lakini ukiwa ni ugonjwa, hapa lazima jasho litakutoka. maisha yako yote ni kuhakikisha unamtimizia vile anavyotaka yeye hatakama vina hasara kwako ukitoka labda unaenda kukutana na marafiki akisema usiende basi anamaanisha usiende la sivyo atanuna.
- Mwanamke mbea
Ukiona mwanamke wako muda wote anataka kujua mambo ya watu wengine, fahamu kwamba huyo hafai.
Asilimia kubwa ya wanawake wa aina hiyo kwani hawawezi kufikiria kuhusu kuboresha nyumba zao, hutumia muda mwingi kufahamu maisha ya watu wengine.
- Mwanamke ambaye hana msimamo
Mwanamke wa aina hii hatakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi katika masuala muhimu hususan yale yanayohitaji usimaizi wake.
Katika dunia ya leo iliyojaa vishawishi vya kila aina, ni vyema mwanaume akawa na mke mwenye msimamo thabiti.
- Mwanamke ‘anayetanguliza’ fedha
Iwapo fedha ndio kipaumbele cha mwanamke huyo, hataweza kukuvumilia katika nyakati zako za dhiki.
Ni vyema mwanamke utakayemchagua akupende wewe katika utu wako, badala ya kupenda fedha zako.