Mwendokasi kwa watakaokwenda SabaSaba

HomeKitaifa

Mwendokasi kwa watakaokwenda SabaSaba

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) imeingia mkataba wa ushirikiano na Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (Dart) utakaowawezesha wananchi watakaokwenda kutembelea Maoesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SabaSaba) kupata huduma za mabasi hayo.

Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade , Latifa Khamisi alisema kupitia ushirikiano huo utakaoanza utekelezaji Juni 27 hadi Julai 14, mwaka huu, wananchi na watu wote wataokwenda kutembelea maonesho hayo watatumia usafiri wa mabasi hayo kuanzia Gerezani hadi vilipo viwanja vya maonesho Barabara ya Kilwa.

“Hatu hii itawafanya wananchi wenye nia ya kuja kutembela maonesho haya kuondokana na usumbufu wa kukosa usafiri wa uhakika kutoka maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na Kibaha,” alisema Khamis.

Kwa upande wa Mtendaji wa Mkuu wa Dart, Edwin Mhede alisema kupitia makubaliano hayo, mamlaka hiyo itahakikisha kunakuwa na huduma za uhakika kwa watembeleaji wa maonesho hayo.

“Katika kuhakikisha suala hilo linatekelezeka, Dart inaweka utaratibu wa kuwa na kadi maalumu kwa ajili ya upandaji wa mabasi hayo, hatua ambayo haitamlazimu abiria kukata tiketi mara kwa mara,” alisema Mhede.

error: Content is protected !!