Rushwa chanzo cha chaguzi CCM kufutwa na kusimamishwa

HomeKitaifa

Rushwa chanzo cha chaguzi CCM kufutwa na kusimamishwa

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amefuta na kusitisha baadhi ya Chaguzi ngazi ya Mikoa kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo rushwa.

“Tumepewa dhamana ya kuratibu, kusimamia na kuhakikisha haki inatendeka, maeneo ambayo tumebaini changamoto tunasimamisha chaguzi kwa ngazi hizo na kwa nafasi ambazo tumebaini changamoto tunafanya uchunguzi wa kina na baada ya kujiridhisha tutachukua hatua,” amesema Chongolo.

Chaguzi zilizofutwa ni pamoja na Chaguzi ya Umoja wa Vijana mkoani Simiyu, nafasi ya mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM – Mbeya na nafasi ya mjumbe wa halmashauri kuu CCM mkoani Arusha.

 

error: Content is protected !!