Namibia, Botswana zafuta sharti la paspoti

HomeKitaifa

Namibia, Botswana zafuta sharti la paspoti

Viongozi wa Botswana na Namibia wametia saini makubaliano ambayo yatawaruhusu raia wao kuvuka mpaka wa nchi hizo mbili bila hitaji la hati za kusafiria — paspoti.

Kuanzia sasa, raia wa nchi hizo mbili za kusini mwa Afrika watahitajika tu kutoa vitambulisho vyao katika maeneo ya kuvuka.

Rais wa Botswana, Mokgweetsi Masisi, na mwenzake wa Namibia, Hage Geingob, walizindua mpango wa kusafiri bila paspoti katika kivuko cha mpaka cha Mamuno.

Masisi alisema kuanzishwa kwa matumizi ya hati za utambulisho kwa usafiri ni muhimu ili kukuza umoja kati ya nchi hizo majirani na mataifa mengine ya kusini mwa Afrika.

error: Content is protected !!