Nape atatua mzozo wa matangazo ya bunge kurushwa

HomeKitaifa

Nape atatua mzozo wa matangazo ya bunge kurushwa

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ameweka wazi hatima ya suala ya matangazo ya Bunge kurushwa mubashara lina haja ya kupitiwa upya lakini liko chini ya mamlaka ya mhimili husika na si serikali.

“Kwa bahati mbaya kwa muda sasa imeshindikana watu kuamini kwamba ufutaji wa Bunge Live halikuwa suala la serikali bali lilikuwa ni suala la bunge lenyewe…Narudia kwa msisitizo suala la urushaji wa matangazo ya bunge ni suala la Bunge lenyewe,” alisema Nape.

Pia alisema, kanuni iliyopo ya utangazaji kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inataka Bunge lenyewe litengeneze utaratibu wa namna ya kurusha matangazo yake. 

Waziri Nape pia alimshukuru Soika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ambaye juzi aliulizwa na waandishi wa habari kuhusu suala hilo na kueleza kuwa linazungumzika na kwamba atajadiliana na serikali kuona namna ya kulifanyia.

error: Content is protected !!