Toleo la 10 la Ripoti ya Furaha Duniani, uchapishaji wa Mtandao wa Sustainable Development Solutions wa Umoja wa Mataifa, umetumia uchanganuzi wa takwimu kubainisha nchi zenye furaha zaidi duniani. Ripoti hiyo inaorodhesha nchi 146 katika furaha zao kwa ujumla na kuangazia ni nchi zipi zilizo na furaha au zisizo na furaha zaidi.
Kwa kutumia matokeo ya Gallup World Poll, Mauritius iliorodheshwa ya kwanza barani Afrika: Ilikuwa na alama ya jumla ya 6.071 kati ya 10, ambayo ilikuwa “mbele kwa kiasi kikubwa” kuliko nchi nyingine zote. Inafaa kukumbuka kuwa Mauritius ikawa nchi ya Kipato cha Juu mnamo Julai 2020, lakini ilirudi kwenye hali yake ya Mapato ya Juu na Kati mnamo 2021 kwa sababu ya janga la ulimwengu la Uviko-19.
Hizi hapa nchi 10 zenye furaha zaidi Barani Afrika.
- Mauritius – 6.071
- Libya – 5.330
- Ivory Coast – 5.235
- South Africa – 5.194
- Gambia – 5.164
- Algeria – 5.122
- Liberia – 5.122
- Congo – 5.075
- Morocco – 5.060
- Mozambique – 5.048
Nchi ambayo haikuwa na furaha zaidi barani Afrika, kulingana na viwango, ilikuwa Zimbabwe, ikiwa na alama 2.995.
Hizi hapa ni nchi 10 zisizo na furaha Barani Afrika.
- Zimbabwe – 2.995
- Rwanda – 3.268
- Botswana – 3.471
- Lesotho – 3.512
- Sierra Leone – 3.574
- Tanzania – 3.502
- Malawi – 3.750
- Zambia – 3.760
- Togo – 4.112
- Mauritania – 4.152