Nini maana ya ugaidi, na gaidi ni nani?

HomeElimu

Nini maana ya ugaidi, na gaidi ni nani?

Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Machi 17, 2005 ulitoa maana ya “ugaidi” kuwa ni kitendo chochote kilichodhamiria kusababisha madhara ua hofu kubwa kwa raia kwa malengo ya kuilazimisha serikali au taasisi za kimataifa kufanya au kuacha jambo fulani. Kwa mfano, mnamo mwaka 1961 ndege ya Marekani ilitekwa nyara na Ramirez Ortiz na kulazimisha ndege hiyo kwenda mji Mkuu wa Cuba, Havana ambapo huko alipewa hifadhi ya kisiasa.

Nchini Tanzania ipo sheria ya kuzuia na kupambana na ugaidi ya mwaka 2002 ambayo ‘Sehemu 2’ imeainisha maana ya ugaidi na kueleza vitendo ambavyo vinaweza kutoa tafsiri ya ugaidi. Moja ya vitendo hivyo ni kusababisha hofu/taharuki kubwa kwenye jamii, kwa njia za makusudi kulazimisha Serikali kufanya au kuacha kufanya jambo fulani, kusababisha uharibifu kwa Serikali na taasisi ya kimataifa, kumteka mtu nyara, kuhatarisha maisha ya mtu n.k (Rejea sheria ya ugaidi ya mwaka 2002).

Ugaidi unaweza kusababisha vifo na taharuki kwa jamii kiasi cha kusababisha kuzorota kwa shughuli za maendeleo katika eneo hilo. Kuonesha namna gani ugaidi sio jambo la mzaha hata kidogo, sheri ya ugaidi ya Tanzania inashughulikia ugaidi kuanzia kwenye hatua ya “nia” (dhamira au azma) ya mtu kutaka kutekeleza vitendo hivyo.

Pale ambapo Jeshi la Polisi “litahisi” au kuona viashiria vya uvunjifu wa amani, basi hatua za awali haraka na zinachukuliwa ikiwamo kumuweka kizuizini mhusika na kutoa matangazo ya tahadhari kwa jamii husika. Zipo tuhuma ambazo hazina dhamana, mojawapo ikiwa ni ya ugaidi. Zipo sababu za msingi kabisa zinazofanya baadhi ya makosa yasiwe na dhamana. moja, ikiwa ni kwa usalama wa mtuhumiwa dhidi yake mwenyewe na dhidi ya raia wenye hasira dhidi yake.

Mtuhumiwa anaweza kufikia uamuzi wa kujitoa uhai wake akiona kuna uwezekano wa yeye kutiwa hatiani, au hata anaweza kuuawa na raia wenye hasira kali kwa minajili ya kulipiza kisasi kwa mtuhumiwa. Sababu nyingine ni kuzuia uwezekano wa mtuhumiwa kuingilia uchunguzi, na sababu ya mwisho ni kuondoa uwezekano wa mtuhumiwa kutoroka nchini kutokana na tuhuma zinazomkabili. Kimsingi tuhuma sio hatia, mtu yeyote anaweza kutiwa hatiani lakini sio lazima kukutwa na tuhuma.

error: Content is protected !!