Ukame na njaa inayoendelea kuutikisa Mkoa wa Arusha na baadhi ya maeneo nchi umewafanya wananchi waliokataa kuhama kwa hiyari kutoka Bonde la Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera katika Wilaya ya Handeni mkoani Tanga kujutia hatua hiyo, kutokana na mifugo kufa kwa njaa kila siku.
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Raymond Mangwala alisema kutokana na ukame wa muda mrefu, idadi ya mifugo inayokufa wilayani humo imeongezeka na kuwa kubwa ikilinganishwa na kpindi kilichopita.
Aliongeza kuwa suluhisho la wafugaji wa Ngorongoro ni kwenda katika maeneo yenye miundombinu imara ya malisho na maji iliyojengwa na serikali Msomera wilayani Handeni.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni, Mashaka Mgeta alisema kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo ya malisho kwa wafugaji wa Msomera na Handeni kwa ujumla yameongezeka na kufanya wafugaji kusahau kupoteza mifugo yao kutokana na ukosefu wa malisho na maji.