Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5

HomeKitaifa

Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5

Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Baraza la Mitihani la Tanzania imekamilisha zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Tano katika shule za sekondari, Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Elimu ya Ufundi vya Serikali Mwaka 2022.

Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Innocent Bashungwa amesema watahiniwa katika mtihani wa Kidato cha Nne kwa mwaka 2021 waliopata Daraja la I hadi III walikuwa 173,422 wakiwemo wasichana 75,056 na wavulana 98,366.

Kati ya wanafunzi hao, wanafunzi wenye sifa ya kujiunga na Kidato cha Tano, vyuo vya Ualimu na vyuo vya Ufundi ni 167,515 wakiwemo wasichana 71,433.

“Idadi hiyo ya wanafunzi wenye sifa imejumuisha wanafunzi wenye mahitaji Maalum 508 wakiwemo wasichana 217 na wavulana 291. Hii ni ongezeko la wanafunzi 19,388 kwa kulinganisha na wanafunzi 148,127 waliokuwa na sifa kwa mwaka 2021,” amesema Waziri Bashungwa.

Orodha ya waliochaguliwa kidato cha Tano na vyuo 2022

error: Content is protected !!