Pweza kufuatiliwa kieletroniki Kilwa

HomeKitaifa

Pweza kufuatiliwa kieletroniki Kilwa

Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa inaanzisha mfumo maalumu wa kufuatilia biashara ya pweza kielektroniki kuanzia wanapovuliwa, kusafirishwa hadi wanapouzwa kupitia madalali.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Eston Ngilangwa wakati akizungumzia hatua zinazochukuliwa kuhakikisha kwamba wilaya hiyo inatumia vyema mpango wa serikali wa uchumi wa buluu ili kutanua soko la samaki pweza na hivyo kuboresha maisha ya wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi huyo alisema hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita kuhusu uchumi wa buluu zimelenga kuhakikisha kwamba samaki wa Tanzania wanapata soko katika soko la kimataifa na kuwa na uvuvi endelevu.

Alisema ili kuwa na soko endelevu na hasa kwa sasa ambapo samaki aina ya pweza wanafanya vyema katika soko la dunia ni lazima nchi kuingia katika mfumo wa ufuatiliaji ili kuhakikisha usalama wa chakula.

Anasema ingawa pweza wa Kilwa wanasoko katika mataifa ya Ufaransa na Ubelgiji, pweza wake wameshindwa kupenya soko kubwa la Japan na Asia kutokana na kukosekana kwa mfumo wa ufuatiliaji wa usalama wa chakula.

error: Content is protected !!