Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Dkt. Tedros Abhanom, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Dunia (WHO) Ikulu, Dodoma leo Januari 20, 2024.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Rais Samia mazungumzo yake na Dkt. Tedros yamejikita haswa katika masuala ya sekta ya afya na jinsi watakavyoweza kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na WHO.
Rais Samia ameeleza juhudi za serikali ya Tanzania katika kupunguza vifo vya watoto wachanga kama ambayo WHO iliagiza.
“Tanzania imezingatia mapendekezo ya WHO ya kuanzisha vitengo vya huduma za watoto wachanga katika hospitali za wilaya ili kufikia asilimia 80 ya hospitali hizo zikiwa na vitengo hivyo.” amesema Rais Samia.
Aidha, ameeleza kuhusu mpango wa Bima ya Afya kwa Wote ambao unafanyiwa kazi ambapo utakapo kamilika Tanzania itakuwa imefanikiwa kutimiza maagizo ya Azimio la Abuja.