Rais Samia afanya uteuzi wa Wakili Mkuu wa Serikali

HomeKitaifa

Rais Samia afanya uteuzi wa Wakili Mkuu wa Serikali

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wakili wa Serikali na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali kama ifuatavyo:

1. Amemteua Dkt. Boniphance Christopher Luhende kuwa Wakili Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi huu Dkt. Luhende alikuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali. Dkt. Luhende anachukua nafasi ya Bwana Gabriel Paschal Malata ambaye aliteuliwa kuwa  Jaji wa Mahakama Kuu.

2. Amemteua Bi. Sarah Duncan Mwaipopo kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi huu Bi Mwaipopo alikuwa Wakili wa Serikali Mkuu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bi. Mwaipopo anachukua nafasu iliyoachwa wazi na Dkt. Luhende ambaye ameteuliwa kuwa Wakili Mkuu wa Serikali.

 

error: Content is protected !!