Rais Samia Suluhu Hassan amelazimika kufupisha ziara yake ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) unaofanyika Dubai na kurejea nchini haraka ili kushughulikia kwa karibu janga la mafuriko mkoani Manyara.
Kutokana na mafuriko yaliyotokea katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang, Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali itagharamia mazishi ya wote waliopoteza maisha pia majeruji wote ambao wapo kwenye hospitali mbalimbali.
Aidha, Rais Samia ameilekeza Serikali ya Mkoa wa Manyara kuhakikisha wananchi wote ambao makazi yao yamesombwa na maji wapate makazi ya muda kwa ajili ya kuwastiri wananchi hao.
Hadi sasa vifo vilivyoripotiwa vimefikia 59 na majeruhi 85. Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa kadri zitakavyoendelea kupatikana.