Rais Samia anadi matumizi ya nishati safi ya kupikia Ufaransa

HomeKitaifa

Rais Samia anadi matumizi ya nishati safi ya kupikia Ufaransa

Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kwenye kuhakikisha suluhisho linapatikana ili kuwezesha upatikanaji wa nishati safi ya kupikia na nafuu barani Afrika.

Rais Samia ametoa msisitizo huo alipokuwa akihutubia katika Mkutano wa Kwanza unaohusu Nishati Safi ya Kupikia Afrika uliofanyika jijini Paris.

Pia, Rais Samia ameeleza nia ya Tanzania ya kuendelea kutetea na kufanyia kazi kwa vitendo mpango wa nishati safi ya kupikia Afrika ili uweze kuwaokoa wanawake pamoja na mazingira kwa ujumla.

“Kutokana na mzigo usio na uwiano unaowakabili wanawake, Tanzania itaendelea kutetea mpango wa nishati safi ya kupikia Afrika sio tu kushughulikia athari za mazingira na afya bali pia kuwawezesha wanawake kama mawakala wa mabadiliko ndani ya jamii zao.” amesema Rais Samia.

Aidha, akihitimisha hotuba yake, Rais Samia amesema kupatikana kwa nishati safi ya kupikia kutawaongezea wanawake nafasi zaidi ya kushiriki katika shughuli za kiuchumi na zenye tija hivyo kuvunja umasikini na utegemezi.

error: Content is protected !!