Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la kuongeza nafasi za ajira 300 katika mamlaka hiyo.
Taarifa ya Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala TRA, Moshi Kabengwe kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda imeeleza ajira hizo ni zile zilizokasimiwa kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026.
Kabengwe alieleza ajira hizo zitajazwa kwenye mchakato uliomalizika hivi karibuni na hivyo kufanya idadi ya watakaoajiriwa kuwa 1,896 badala ya 1,596 ya awali.
TRA ilimshukuru Rais Samia kwa kuridhia ombi hilo la kuongeza nafasi hizo za ajira.