Rais Samia atoa bilioni 2 Ruangwa

HomeKitaifa

Rais Samia atoa bilioni 2 Ruangwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Kata ya Nanganga wilayani Ruangwa ikiwamo ya afya, elimu na maji.

Akizungumza jana akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi hiyo kuwa serikali imetoa sh.milioni 447 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa usambazaji maji Nanganga, Sh. milioni 31 ya kusambaza katika kijiji cha Mbecha na Sh. milioni 470 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mchenganyumba.

“Rais Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajii ya ujenzi wa mradi wa umwagiliaji Nanganga, tutumie vizuri bonde letu, vijana changamkieni fursa hii kwa kuanzisha kilimo cha mboga na mazao mengine,”alishauri Waziri Majaliwa.

Aidha, aliuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kuendelea na mpango wa ujenzi wa solo la mboga katika Kata ya Nanganga ili kuwawezesha wakulima wa mazao hayo kupata sehemu ya uhakika ya kufanyia biashara.

 

error: Content is protected !!