Rais Samia atoa maagizo kwa serikali za mitaa

HomeKitaifa

Rais Samia atoa maagizo kwa serikali za mitaa

Rais Samia Suluhu ameongoza ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT), uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma.

Rais ameeleza kuwa serikali inatambua kwamba serikali za mitaa ni nguzo na injini ya maendeleo katika nchi hii kwa sababu zipo karibu na wananchi na pia kuwa kiungo kikubwa kati ya wananchi na serikali.

Katika hotuba yake Rais amewataka viongozi watakaochaguliwa kuweka kipaumbele mambo ya msingi na yenye manufaa katika maendeleo ya nchi hii na sio vinginevyo. Amewataka viongozi hao kusambaza habari na kutoa ushauri kwa serikali za mitaa, kutumia mitandao katika kutoa huduma, ukusanyaji wa mapato na uwekaji wa takwimu.

Aidha, ameeleza kuwa viongozi watakaochaguliwa waweke kipaumbele suala zima la kuwepo kwa mijadala na utetezi wa sera na sheria za serikali zinasohusu serikali za mitaa katika kuteleza malengo endelevu.

Rais pia amewataka viongozi hao kuhakikisha kuwa miradi iendane na thamani ya fedha zinazotolewa na serikali na pia ushirikishwaji wa wananchi katika maendeleo.

Mwisho kabisa Rais ametoa agizo kwa viongozi watakaochaguliwa kusimamia na kuyatekeleza mambo hayo aliyoyaeleza kama kipaumbele katika kuleta maendeleo endelevu hapa nchini.

error: Content is protected !!