Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu, ametengua wakurugenzi wanne ikiwemo Buchosa, Singida mjini, Mbeya na Iringa kutokana na ubadhirifu wa pesa za ujenzi wa madarasa zilizotokana na mkopo wa UVIKO-19.
Rais Samia amesema tayari ameshaweka timu yake ambayo itamsaidia kujua mwenedo wote wa matumizi ya pesa hizo kwenye ujenzi wa madarasa.Rais Samia ameyasema hayo leo aliposimama kuongea na wanachi katika Wilaya ya Magu, Mkoani Mwanza akielekea Musoma kwenye maadhimisho ya miaka 45 ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Sambamba na hayo alimsisitizia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa ameagizwa kuendelea na uchunguzi katika wilaya ya Geita.
Aidha pia Rais Samia alikumbushia kauli yake kabla ya kuanza kwa utekelezaji wa miradi hiyo kuwa endapo kuna mkurugenzi anataka kuziona rangi zake basi acheze na pesa hizo ambazo zilitolewa kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu nchi nzima.