Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua Kiwanda cha Chokaa na Saruji- Maweni Limestone mkoani Tanga na kuzungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho.
Katika ufunguzi wa kiwanda hicho, Rais Samia amewapongeza wafanyakazi kwa kufanya kazi katika kiwanda hicho na pia kwa wawekezaji waliokwenda kuwekeza katika eneo hilo.
Aidha, Rais Samia amewasihi wawekezaji wote kulipa kodi na tozo za serikali ili ziweze kuwezesha wananchi kupata maendeleo na huduma za kijamii.
“Niwasihi wawekezaji wote kama mnavyolipa kodi na tozo za Serikali kuu, hakikisheni mnalipa pia ushuru wa Halmashauri. Serikali za Mitaa ni mamlaka halali kisheria na zinategemewa sana na wananchi kwa maendeleo, hivyo ni muhimu kukawa na ushirikiano mzuri na wa karibu baina ya wawekezaji na halmashauri husika ili tuharakishe maendeleo.” – Rais Samia Suluhu akifungua Kiwanda cha Saruji, Tanga
Akimalizia hotuba yake, Rais Samia ametoa wito kwa wananchi wa Tanga kutumia saruji inayozalishwa mkoani humo kujinufaisha kwa kuboresha makazi yao na kuipa hadhi mkoa huo.