Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan ameelekeza Jumuiya ya Wanawake UWT kuongeza Nguvu katika kupata wanachama wapya na kusimamia Vizuri miradi ya Jumuiya hiyo ili kujiimarisha kiuchumi.
Rais Samia amesema hayo kwenye Ufunguzi wa Mkutano wa 10 wa Jumuiya ya Wanawake CCM Taifa UWT uliokwenda sambamba na uchaguzi wa Viongozi wa Jumuiya hiyo ambapo jumla ya Wajumbe 802 Kati 830 wamehudhuria Mkutano huo.
Aidha,Rais Samia ameelekeza Jumuiya zote za Chama Cha Mapinduzi kuvunja Makundi kwakuwa uchaguzi wa Viongozi na Wajumbe wa Jumuiya hizo umemalizika na Sasa ni wakati wa kukijenga Chama kwa Pamoja.
Pamoja na hayo Rais Samia amewataka wanachama na Viongozi wa Chama hicho kukitumikia Chama na sio kutumikia mtu mmojammoja huku akitaka Jumuiya kushirikiana.
Katika Mkutano huo, Rais Samia ameelezea Miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ambapo ametoa wito kwa Viongozi wa Chama kuisemea miradi inayotekelezwa kwenye maeneo yao Ili Wananchi wa eneo husika wafahamu.
Hata hivyo Rais Samia amezipongeza Jumuiya zote za Chama hicho kwa kumaliza uchaguzi salama na kupata Viongozi wanaowahitaji.