Rais Samia Suluhu Hassan anaanza ziara ya kiserikali ya siku tatu nchini Cuba yenye lengo la kuimarisha uhusiano baina ya mataifa hayo mawili.
Ziara hiyo inalenga kuziwezesha nchi hizo kuendelea kukuza uhusiano wake kihistoria na kideplomasia kuwa wa kimkakati kwa kufungua maeneo mapya ya ushirikiano yenye maslahi kiuchumi pamoja na kijamii.
Aidha, Novemba 8, 2024 Rais Samia atakuwa mgeni rasmi na kufungua kongamano la Kimataifa la Kiswahili litakalofanyika nchini humo.
Tanzania na Cuba ni washirika wa muda mrefu tangu enzi ya ukombozi wa Bara la Afrika ambapo ushirikiano huo umeziwezesha nchi hizo kuendelea kusimama pamoja ikiwemo kuichagua Cuba kuwa mwenyeji wa Kongamano hilo