Kuanzia mwezi Agosti, 2024 Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC.
Nafasi hii itaiwezesha Tanzania kuratibu, kusimamia na kuongoza majadiliano na maamuzi yote yanayohusu masuala ya siasa, ulinzi na usalama.
Aidha, nafasi hii itaimarisha ushawishi wake katika ukanda wa SADC katika masuala haya hasa ikizingatiwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa Waasisi wa SADC walioshiriki kwa hali na mali katika harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika.