Rais wa shirikisho la soka Tanzania( TFF) Wallace Karia ametangaza udhamini uliotolewa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan wa mashindano ya Afrika Mashariki na kati (CECAFA) kwa upande wa wanawake.
Karia ameeleza kuwa Rais Samia atatoa zawadi ya jumla ya dola za Marekani 60,000 ambapo bingwa atapata dola 30,000 mshindi wa pili dola 20,000 mshindi wa tatu dola 10,000.
Mashindano hayo kwa upande wa wanaume yanadhaminiwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame.