Rais Samia : Mpikie gesi

HomeKitaifa

Rais Samia : Mpikie gesi

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua  nyumba 644 za Magomeni , Dar es Salaam ambazo ujenzi wake umegharimu TZS bilioni 52.2 na kuwasihi wakazi wa kota hizo kuwa wasafi na kulinda majengo hayo.

“Nawaomba matunzo katika nyumba hizi ikiwemo usafi, usafi wa nyumba dhamana iko kwenu. Nyumba kama hizi tunategemea watu mpikie gesi na hatutegemei mtatumia kuni,” alisema Rais Samia Suluhu.

Katika uzinduzi huo, Rais Samia ameridhia ombi la wananchi waliokuwa wanataka kuuziwa nyumba hizo na kuwaambia kuwa wanaweza kuanza kulipa kidogo kidogo bila kutoa gharama  ya ardhi.

“Nimeridhia wananchi kuuziwa nyumba [za Magomeni Kota] kwa utaratibu wa mpangaji mnunuzi, na kurejesha gharama za nyumba pekee. Hatutawatoza gharama ya ardhi kwa sababu tukifanya hivyo, mtashindwa kuzinunua.” alisema Rais Samia Suluhu.

Aidha, Rais Samia ameahidi kutekeleza miradi yote iliyoanzishwa na kuachwa na Hayati Magufuli huku akiwataka wale waliohisi kuwa atashindwa kuondoa fikra hiyo kwani atakeleza kwa manufaa ya Watanzania.

“Nitatekeleza miradi yote iliyoachwa na mtangulizi wangu, waliokuwa wanahisi kwamba sitaweza kutekeleza pengine hekima haikutumika, kwa kuwa miradi hii ni utekelezaji wa Ilani na tunatekeleza kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania,” alisema Rais Samia Suluhu.

error: Content is protected !!