Rais Samia Suluhu atunukiwa Tuzo ya Heshima ya Maji

HomeKitaifa

Rais Samia Suluhu atunukiwa Tuzo ya Heshima ya Maji

Rais Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Tuzo ya Juu ya Heshima ya Maji ‘Presidential Global Water Changemakers Awards 2025’ iliyotolewa na Global Water Partnerships kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika.

Tuzo hiyo imetolewa leo Jumatano Agosti 13, 2025 na Rais, Duma Boko wa Jamhuri ya Botswana, ambaye ni Mwenyekiti wa “Presidential Global Water Changemakers Awards 2025” na kupokewa kwa niaba yake na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, James Bwana.

Tuzo hiyo imetolewa wakati wa mkutano wa uwekezaji katika Sekta ya Maji Barani Afrika, ulioanza leo jijini Cape Town – Afrika Kusini na utahitimishwa Agosti 15, 2025.

Home

Rais huyo amesema, “Global Water Partnerships inatambua mchango mkubwa wa Rais Samia katika uongozi na mageuzi kwenye Sekta ya Maji ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya maji, usambazaji maji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na ubunifu wa kutafuta fedha za maji kupitia Hati Fungani ya Kijani (Green Bond) iliyotolewa na Mamlaka ya Maji Tanga.”

Viongozi wengine waliotunukiwa tuzo hiyo ni Cyril Ramaphosa, Rais wa Afrika Kusini; Bassirou Diomaye Faye wa Senegal; Mtukufu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan, Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mohammed bin Salman Al Saudi, Mwanafalme na Waziri Mkuu wa Falme ya Saudi Arabia na Mtukufu Mfalme Letsie III wa Falme ya Lesotho.

Katika mkutano huo, Rais mstaafu, Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Jopo la Viongozi Mashuhuri katika Uwekezaji kwenye Sekta ya Maji Barani Afrika, anashiriki pia.

error: Content is protected !!