Avance Media imetangaza orodha ya Wanawake 100 Wenye Ushawishi Mkubwa Barani Afrika kwa mwaka 2025, chapisho ambalo linatambua wanawake wa Kiafrika ambao uongozi, ushawishi na mafanikio yao yanaendelea kuathiri maamuzi katika ngazi za juu kitaifa na kimataifa.
Miongoni mwao ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo chapisho hilo limetambua na kumuenzi kwa mchango wake mkubwa na wa kipekee, ambao unaendelea kuhamasisha na kufungua fursa mpya kwa wanawake wa Kiafrika barani Afrika na katika diaspora.
Kupitia uongozi wake wa mfano katika sekta ya utawala, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anaakisi kwa vitendo ushawishi wa wanawake wa Kiafrika katika kuunda sera, kuathiri utamaduni, kuhimiza ubunifu, na kuchagiza mustakabali wa bara la Afrika.
View this post on Instagram


