Rais Samia Suluhu na Papa Francis kuendeleza uhusiano wa Tanzania na Vatican

HomeKitaifa

Rais Samia Suluhu na Papa Francis kuendeleza uhusiano wa Tanzania na Vatican

Rais Samia Suluhu amekutana na Papa Francis leo Februari 12,2024 San Damaso mjini Vatican na kufanya mazunguko ya faragha.

Pia Rais Samia alikutana na Katibu wa Vatican wa Mambo ya Nchi, Kardinali Pietro Parolin na Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mashirika ya Kimataifa, Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher.

Mazungumzo kati ya Rais Samia na Papa Francis yalijikita katika kuendelea mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Vatican na pia namna ambavyo Kanisa Katoliki limekuwa likishughulikia masuala ya maendeleo katika maeneo ya hisani, elimu na afya.

Aidha, mwisho wa mazungumzo hayo pande zote mbili zimekubaliana kuendeleza ushirikiano wa muda mrefu na kuendelea kukuza amani.

error: Content is protected !!