Usichaji simu hadi asilimia 100

HomeElimu

Usichaji simu hadi asilimia 100

Huenda watumiaji wa simu za mkononi za iPhone zinazotengenezwa na kampuni ya Apple wakaepuka gharama za kununua au kutengeneza betri za simu yao mara kwa mara baada ya kampuni hiyo kushauri kutochaji simu zao mpaka asilimia 100  kama njia mojawapo ya kutunza uhai wa betri kwa muda mrefu.

Hivi sasa Simu ya mkononi imekuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku  na ili uweze kutumia lazima iwe imechajiwa, ambapo baadhi ya watumiaji huchaji simu zao kila siku kulingana na matumizi yao na baadhi wamekuwa wakiacha simu zao zinachajiwa usiku mzima ili asubuhi wakute zimejaa.

Hata hivyo, kuchaji simu ya iPhone mpaka asilimia 100 kunaweza kusiwe afya kwa betri ya simu yako kwani kunapunguza uwezo wa betri siku baada ya siku.

Apple katika taarifa yake iliyotolewa wiki hii, imeeleza kuwa betri la simu lina madini ya Lithium-ion ambayo huathiriwa ikiwa yatapata kiwango kikubwa cha umeme.

Kuweza kutambua kama betri ya simu imeathiriwa unaweza kuangalia katika mpangilio wa simu yako katika sehemu ya  afya ya betri na ukiona imepungua, njia unayoweza kutumia ili kuepuka uharibifu zaidi ni kuitoa kwenye chaji kila inapofikia asilimia 80.

Aidha, njia nyingine unayoweza kutumia ni kuruhusu kiwango kidogo cha chaji kuendelea kuingia kwenye betri pale inapofikia asilimia 80, mpangilio ambao hujiweka wenyewe kwenye simu za iphone 13.

Kwa mujibu wa gazeti la The Guardian, muda wa matumizi ya betri ni muda ambao kifaa chako hufanya kazi kabla ya kuhitaji kuchajiwa upya na maisha ya betri ni muda ambao betri yako hudumu hadi inapohitajika kubadilishwa,

“Zingatia  vyote viwili na utapata manufaa zaidi kutoka kwa vifaa vyako vya Apple, haijalishi unamiliki vipi,” inaeleza sehemu ya habari ya gazeti hilo kuhusu Apple.

Pamoja na kuhakikisha iPhone yako haichaji mara kwa mara hadi asilimia 100, kuna hatua chache muhimu unazoweza kuchukua ili kuongeza maisha ya betri na maisha yako.

Watumiaji wa iPhone wanapaswa kutunza simu zao katika sehemu yenye joto kati ya juzijoto 16 hadi 22 na haitakiwi kuzidi nyuzijoto 35. Hivyo, epuka kuiweka  iPhone yako juani au kuichaji  chini ya mto.

Inafaa pia kuweka mipangilio inayoruhusu umeme mdogo kutumika ndani ya simu hii itapunguza mwangaza wa skrini na kurekebisha vyema shughuli za kifaa chako na kukifanya kidumu kwa muda mrefu.

error: Content is protected !!