Rais Samia: Tuna kazi kubwa ya kuendeleza umoja na mshikamano

HomeKitaifa

Rais Samia: Tuna kazi kubwa ya kuendeleza umoja na mshikamano

Rais Samia Suluhu amesema Maalim Seif amewaachia Watanzania kazi kubwa ya kuendeleza umoja na mshikamano.

Rais Samia ameeleza hayo wakati ya Hotuba yake kama mgeni rasmi Katika mkutano wa Maadhimisho ya Maisha ya Maalim Seif Sharif Hamad uliofanyika leo Oktoba 5 katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema, hayati Maalim Seif alikua na utayari wa kuzungumza inapotokea utofauti katika siasa akitolea mfano hali ilivyokuwa  baada ya Uchaguzi Mkuu 2000, ambapo Maalim Seif alikuwa sehemu muhimu ya muafaka kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Wananchi ‘CUF’.

Rais Samia amesema pamoja na msukumo ambao Maalim Seif alikua anaupata kutoka kwa vyama vingine, lakini bado alichagua njia sahihi ya maridhiano iliyopelekea amani na mshikamano visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Rais Samia amesisitiza kwamba namna nzuri ya kumuenzi Maalim Seif ni kudumisha amani na mshikamano na kutumia njia ya vikao vya maridhiano pale zinapotokea tofauti.

Kubwa zaidi katika sghuli hiyo, Rais Sami Suluhu amezindua taasisi ya Maalim Seif na kusema kwamba ni lazima watu washirikiane kuindeleza Tasisi hiyo bila kuegemea kwenye chama chochote cha kisiasa.

error: Content is protected !!