Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Daniel Francisco Chapo anatarajia kuanza Ziara ya Kiserikali ya siku tatu hapa nchini kuanzia leo tarehe 07 Mei, 2025, kufuatia mwaliko wa Rais Samia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hii ni ziara ya kwanza ya kiserikali ya Mhe. Rais Daniel Chapo kuifanya nchini Tanzania tangu aapishwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Msumbiji tarehe 15 Januari, 2025.
Ziara hii itadumisha mahusiano yaliyopo, kuimarisha ushirikiano kwenye sekta mbalimbali pamoja na kufungua fursa mpya za ushirikiano zenye maslahi kwa pande zote mbili.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI pic.twitter.com/9euMuVzIFl
— ikulu_Tanzania (@ikulumawasliano) May 7, 2025