Walioomba Sensa wapita idadi inayohitajika

HomeKitaifa

Walioomba Sensa wapita idadi inayohitajika

Watu 674,484 wameomba nafasi za ajira za muda za Sensa ya Watu na Makazi ikiwa imezidi idadi kamili inayohitaji kwa ajili ya shughuli hiyo ni 205,000.

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi, Anna Makinda alisema kati ya hao walioomba, waliofanikisha kukamilisha maombi ni 575,672.

“Mpaka tulipopata takwimu za saa nne (juzi) walikuwapo walioomba kama 674,484, lakini waliohitimsha zoezi zima ni 575,672. Kwa hiyo watu 98,812 naona safari haikufika mwisho,” alisema Makinda.

Alibainisha kuwa baada ya zoezi hilo, kutakuwa na usaili mdogo ambao utafanyika ana kwa ana na kueleza kwamba mchakato huo utachukua siku zaidi ya 10 na baada ya  hapo, waliochaguliwa wataingia kwenye mafunzo ya kwa takribani siku 21.

error: Content is protected !!