Rais Samia amaliza mgogoro uliodumu kwa miaka 22 Mtwara

HomeKitaifa

Rais Samia amaliza mgogoro uliodumu kwa miaka 22 Mtwara

Rais Samia Suluhu Hassan ameidhinisha malipo ya Sh milioni 816.7 ikiwa ni fidia kwa wananchi wa Mangamba Juu manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara akimaliza mgogoro uliodumu kwa karibu miaka 22.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Danstan Kyobya ametoa amesema watakao nufaika ni wananchi walitoa eneo lao miaka 22 iliyopita kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mtwara (MTUWASA) kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji.

“Mheshimiwa Rais ameleta Shilingi milioni 816.78 ambazo zitalipwa kama fidia ya eneo lililochukuliwa kuruhuisu ujenzi wa miundombinu ya maji ya MTUWASA hapa Mtwara,” amesema.

error: Content is protected !!