Rorya yatumia milioni 99 kwa ajili ya mikopo 10%

HomeKitaifa

Rorya yatumia milioni 99 kwa ajili ya mikopo 10%

Halmashauri ya Wilaya ya Rorya mkoani Mara imetoa Shilingi milioni 99 kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali la kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa makundi maalumu.

Akizungumza wakati wa kukabidhi fedha hizo kwa vikundi 17 vilivyonufaika, Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri hiyo, Cosmas Mwatisya alisema fedha hizo zilitokana na mapato ya robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024.2025.

“Lengo ni kusaidia makundi haya kujitegemea kiuchumi na kuchangia maendeleo ya jamuu zao. Fedha hizi zinapaswa kurejeshwa kulingana na masharti waliyopewa,”alisema.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Abdul Mtaka alisema mikopo hiyo haina riba na imelenga kumwezesha mlengwa kutimiza malengo yake bila kikwazo.

“Tunawaomba wanufaika kutumia mikopo hii kwa makusudi yaliyokusudiwa, hatuwezi kuruhusu fedha hizi kupotea kwa matumizi yasiyo na tija,” aliongeza Mtaka.

error: Content is protected !!