Rugemeleza: Lissu ataanza mgomo wa kutokula kuanzia Jumatatu

HomeKitaifa

Rugemeleza: Lissu ataanza mgomo wa kutokula kuanzia Jumatatu

Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Rugemeleza Nshala amesema Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu amesema kuanzia Jumatatu Oktoba 26, 2026 ataanza mgomo wa kutokula chakula baada ya kunyimwa haki yake ya kukutana na mawakili.

Dkt. Nshala amesema uamuzi wa Lissu unakuja kufuatia uongozi wa Gereza la Ukonga kueleza kuwa utaratibu utatumika kama ule uliokataliwa na Mahakama kwamba Naibu mkuu wa gereza, mwanasheria na maafisa wengine watakuwepo katika chumba wanachozungumza na Lissu.

Ameongeza kuwa Lissu alikataa kuzungumza na mawakili wake ambao ni Nashon Nkungu na Paul Kisabo waliofika kwenye gereza hilo akisema utaratibu ulioagizwa na Mahakama kuwa maafisa wakae umbali wanaoweza kuona na sio kusikia umekiukwa.

error: Content is protected !!