Sababu ya matuta mengi ‘Kilwa Road’

HomeKitaifa

Sababu ya matuta mengi ‘Kilwa Road’

Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) umesema matuta yaliyowekwa katika Barabara ya Kilwa mkoani Dar es Salaam siyo  ya kudumu, bali yanalenga kupunguza vifo vya wanafunzi na ulemavu uliokuwa ukisababishwa na madereva wasio waadilifu.

Meneja wa TANROADS mkoa wa Dar es Salaam, Harun Senkuku, alisema matuta hayo hayatatumika kwa muda mrefu, hivyo akawataka watumiaji wa barabara waendelee kuvumilia mpaka mkandarasi atakapokamilisha ujenzi.

“Kesi za watoto wa shule (wanafunzi) kugongwa zilikuwa nyingi katika eneo lile, hivyo ikatulazimu kuja na mbinu mbadala ya kuokoa maisha ya watoto wale.

“Ni kweli kuna foleni lakini wavumilie mkandarasi amalize kazi, tuhamie hatua nyingine,” Meneja huyo alifafanua.

Senkuku aliongeza kuwa TANROADS inatambua kuwa matuta yameongeza foleni kwa kupunguza kasi ya magari, hivyo akaahidi kuwa ujenzi ukikamilika, yataondolewa na kuwekwa taa za barabarani ambazo zitasaidia kupunguza ajali.

error: Content is protected !!