Sababu za ACT kushiriki kikao kilichogomewa na CHADEMA

HomeKitaifa

Sababu za ACT kushiriki kikao kilichogomewa na CHADEMA

Chama cha siasa cha ‘Alliance for Change and Transparency’ (ACT-Wazalendo) kimesema kitashiriki katika kikao cha wadau wa tasnia ya siasa kupitia Baraza la Vyama vya Siasa kinachotarajiwa kufanyika jijini Dodoma kuanzia kesho Desemba 15,2021 hadi Desemba 17,2021

Kikao hicho, ‘kimegomewa’ na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambapo Desemba 12, 2021, Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika, alieleza kwamba CHADEMA hawatashiriki.

Kwa upande wa ACT-Wazalendo, wamesema watashiriki kikao hicho wakiwakilishwa na Kiongozi wao Zitto Kabwe, Kaimu Mwenyekiti wa ACT  Taifa Dorothy Temu, Katibu Mkuu wa ACT Ado Shaibu na Mwanasheria wao Omary Said Shaaban.

ACT wameeleza sababu zitakazowafanya washiriki kikao hicho, wakisema sababu ya kwanza kudai mabadiliko ya Kikatiba na Kisheria kuhakikisha kwamba chaguzi nchini zinakuwa huru, za haki na zenye kuaminika.

Sababu ya pili ni ACT  kutaka kuandikwa upya kwa Sheria ya Vyama vya Siasa ili kuhakikisha  Vyama vyote vya Siasa nchini vinafanya shughuli zake kwa uhuru na usawa.

ACT wamesema sababu nyingine ni kutaka maboresho ya Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili vifanye kazi zake kwa weledi haki na uhuru na sababu ya mwisho ni kutaka Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe aachiwe huru.

error: Content is protected !!