Sababu za Air Tanzania kupunguza miruko

HomeKitaifa

Sababu za Air Tanzania kupunguza miruko

Taarifa iliyotolewa na Kampuni ya Ndege ya Air Tanzania (ATCL) imesema “Kutokana na changamoto za kiufundi kote duniani za injini aina ya PW1524G-3 zinazotumika katika ndege za Airbus A220-300 na kwa kuzingatia matakwa ya usalama, tumekuwa tukifuata maelekezo ya kitaalam ili kutoa huduma bora na ya usalama.

Na wakati mwingine tunazitoa ndege katika mzunguko kukidhi matakwa ya watengenezaji wa injini hizi.

Hatua hizi zimesababisha ucheleweshaji wa ndege zetu wakati changamoto hii ikitafutiwa ufumbuzi.

Ili kuhakikisha ndege zetu zinafanya kazi kufuatana na ratiba, tutapunguza miruko na kufuta baadhi ya safari zetu kulingana na idadi ya ndege zilizopo.

Uamuzi huu ni wa muda mfupi ili kutoa muda kwa watengenezaji wa injini hizo kushughulikia matatizo yaliyopo. Tunaomba radhi kwa usumbufu uliokuwa umejitokeza na utakaojitokeza kutokana na mabadiliko katika ratiba zetu.

error: Content is protected !!