Sabaya ashinda kesi

HomeKitaifa

Sabaya ashinda kesi

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake sita katika kesi ya uhujumu uchumi namba ishirini na saba ya mwaka 2021 kutokana na hati ya mashtaka kuwa na mapungufu pamoja na ushahidi kugubikwa na maswali mengi.

Hii ni kesi ya pili ambayo Lengai Ole Sabaya anashinda dhidi ya Jamhuri baada ya awali kushinda rufaa ya kesi ya jinai namba 105 ya mwaka 2021 ambayo ilitolewa Mei 06, 2022 ambapo kwenye rufaa hiyo Sabaya alikuwa pamoja na wenzake wawili; Sylvester Nyegu na Daniel Mbura.

Hata hivyo Sabaya ataendelea kubaki rumande kutokana na kukabiliwa na kesi nyingine mkoani Kimanjaro.

error: Content is protected !!