Sabaya jela miaka 30

HomeKitaifa

Sabaya jela miaka 30

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha. Kabla ya kuhukumiwa Sabaya alipewa nafasi ya kujitetea na kutoa utetezi wake kwa kusema  sio yeye alifanya hivyo ila alikua anatimiza maagizo ya serikali na pia ana mchumba ambaye anataka kumuoa na tayari ameshatoa mahari tayari kwa kumuoa mchumba wake.

Hakimu mkazi mwandamizi wa Mahakama ya Arusha akitolea ufafanuzi hukumu hiyo, amesema kuwa imethibitika mshitakiwa wa kwanza alikuwa na bastola ndani na nje kulikuwa na watu wawili wenye silaha hivyo, hakuna shaka duka la shahidi wa kwanza lilivamiwa na watu wenye silaha na lilikuwa chini ya watu wenye silaha.

> Wasifu wa Lengai Ole Sabaya

Hata hivyo, amesema hakuna silaha iliyotumika katika tukio hilo, hivyo hakuna shambulizi la kutumia silaha, aidha Hakimu amesema kati ya mashahidi 11 waliotoa ushahidi wao dhidi ya Sabaya, ni mashaidi wawili tu ndio ambao ushahidi wao haukuwa na mashiko.

error: Content is protected !!