Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne leo Jumatatu Juni 20, 2022 wamefikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi kusikiliza mashtaka yanayowakabili ikiwemo uhujumu uchumi.
Juni 7, 2022 mahakama hiyo iliahirisha kesi hiyo baada ya upande wa mashtaka kueleza kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Kesi hiyo namba mbili ya mwaka 2022 inayosikilizwa na hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Salome Mshasha imekuja kwa ajili ya kutajwa.