Shirika la Reli Tanzania na Zambia (TAZARA) limetangaza kurejea kwa safari za treni za abiria kutoka Dar es Salaam kwenda New Kapiri Mposhi nchini Zambia kuanzia Februari 10, mwaka huu.
Hatua hiyo imekuja baada ya kukamilika kwa maboresho na marekebisho mbalimbali ya kiufundi na kiutendaji yaliyolenga kuboresha huduma za treni za abiria zinazovuka mipaka kati ya Tanzania na Zambia.
Safari hizo zilikuwa zimesitishwa tangu Juni 2024 kutokana na changamoto mbalimbali.


