Sensa kutoa majibu vifo vya wajawazito

HomeKimataifa

Sensa kutoa majibu vifo vya wajawazito

Waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema kuwa sensa ya mwaka huu inakwenda kutoa majibu ya ukubwa wa tatizo la vifo vya wajawazito na watoto wa changa.

Hayo ameyasema wakati akifunga bonaza la michezo mbalimbali lililokuwa na lengo la kutoa elimu na hamasa Kwa wananchi kushiriki katika zoezi la sensa.

Amesema kuwa licha ya kuwepo Kwa takwimu za vifo hivyo hapa nchini lakini sensa inakwenda kubainisha ukubwa wa changamoto hiyo.

“Niwaombe wananchi wa Jiji la Tanga tuhakikishe tunatoa ushirikiano kwa makarani wa sensa watakapopita katika maeneo yetu kwa kutoa taarifa sahihi “amesema Waziri Ummy.

error: Content is protected !!