Serikali kuendelea kuwapima wanafunzi mimba

HomeKitaifa

Serikali kuendelea kuwapima wanafunzi mimba

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omari Kipanga amesema utaratibu wa kuwapima mimba wanafunzi wanapotoka likizo unaendelea katika shule mbalimbali za sekondari nchini.

Kauli hiyo ameitoa wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Songwe, Philip Mlugo (CCM) aliyehoji kwanini serikali isiendelee na utaratibu wa kuwapima mimba wanafunzi wa darasa la sita, saba na wale sekondari ili kupunguza tatizo la mimba za utotoni.

Kipanga amesema utaratibu huo wa kuwapima wanafunzi wakitoka likizo upo na unaendelea shuleni lakini hautangazwi hadharani.

error: Content is protected !!