Serikali kushirikiana na sekta binafsi ujenzi wa barabara ya haraka

HomeKitaifa

Serikali kushirikiana na sekta binafsi ujenzi wa barabara ya haraka

Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi inakusudia kujenga barabara ya haraka (express way) kutoka Kibaha hadi Morogoro ambayo itakuwa ya kulipia. Waziri wa Ujenzi, Prof. Makame Mbarawa amesema kwa ambao hawatoweza kulipia watatumia barabara ya kawaida iliyopo sasa.

“Serikali tumejipanga kushirikiana na sekta binafsi katika ujenzi wa barabara mpya ya Kibaha-Chalinze-Morogoro kilomita 215 (express way), ambapo mkandarasi atajenga kwa fedha yake na watakaotumia barabara hiyo watalipia,” amesema Prof. Mbarawa.

 

error: Content is protected !!