Serikali yasema itaendelea kupunguza tozo

HomeKitaifa

Serikali yasema itaendelea kupunguza tozo

Waziri wa Fedha na Mipango amesema kuwa huko mbeleni wakati sekta ya elimu imeimarika, serikali itapitia tena tozo zinazokatwa ili kuboresha sekta hiyo na nyinginezo.

Dkt. Mwigulu Nchemba amesema hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu punguzo la asilimia za makato lililotangazwa na serikali Agosti 31, 2021, na kufafanua kuwa watoto wengi wanaomaliza elimu ya msingi wamekuwa wkaikosa fursa ya kuendelea na msomo ya elimu ya sekondari.

Amesema hakuna haja ya wananchi kubeba suala la makato kama ugomvi, kwani dhima ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha fedha hizo zinarudi kuwahudumia wananchi.

Amewataka Watanzania wamwamini Rais kwani ana dira nzuri ya maendeleo na kwamba hilo kufanikiwa ni lazima wananchi wote washiriki.

Ametumia mkutano huo kuwataka Watanzania kuacha hulka ya kusbiri tatizo litokee ndipo waanze kuwaza namna ya kulitatua, na kwamba Rais yeye ameamua kutatua tatizo kabla halijatokea.

error: Content is protected !!