Serikali yatangaza miradi sita mikubwa ya barabara kwa ubia na sekta binafsi

HomeKitaifa

Serikali yatangaza miradi sita mikubwa ya barabara kwa ubia na sekta binafsi

Serikali imefungua fursa mpya za uwekezaji katika sekta ya miundombinu kwa kutangaza miradi mikubwa ya barabara itakayotekelezwa kupitia ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP), hatua inayolenga kuvutia mtaji wa wawekezaji na kupunguza utegemezi wa fedha za bajeti ya serikali.

Kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), fursa hizo zinahusisha miradi sita ya kimkakati ikiwemo upanuzi wa barabara za Morogoro–Dodoma, Chalinze–Segera–Tanga na Handeni–Kiberashi–Chemba–Kwamtoro–Singida, pamoja na ujenzi wa Expressway ya Dar es Salaam–Kibaha, Expressway ya Katikati ya Jiji hadi Uwanja wa Ndege wa JNIA na maboresho ya Mteremko wa Kitonga.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha PPP, David Kafulila, amesema hatua ya kutangaza miradi hiyo kwa uwazi ndani na nje ya nchi itapanua ushindani miongoni mwa wawekezaji na kuongeza fursa za upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Wawekezaji watakaopatikana watashiriki katika kubuni, kugharamia, kujenga, kuendesha na kutunza miundombinu hiyo kabla ya kuikabidhi kwa serikali kwa mujibu wa masharti ya mikataba ya ubia.

error: Content is protected !!