Bei mpya za mafuta mwezi Oktoba

HomeBiashara

Bei mpya za mafuta mwezi Oktoba

Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei mpya ya mafuta ya petroli kupanda kwa Sh.12 badala ya Sh.145 ambayo ilitakiwa kutozwa kwa lita kuanzia kesho.

Mhandisi Godfrey Chibulunje, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA amesema hayo leo jijini Dodoma alipokuwa akitoa ufafanuzi wa tozo hizo nane na kutangaza bei mpya za mafuta kwa Mwezi Oktoba ambazo zitaanza kutozwa kuanzia Oktoba 6, 2021.

 > Kauli ya Rais Samia kuhusu tozo

Aidha, ameainisha bei elekezi kwa baadhi ya mikoa, Dar es salaam lita ya mafuta ya petroli ni Sh.2,439, dizeli Sh. 2,261, mafuta ya taa Sh.2,188, Kwa Arusha lita ya Petroli ni Sh.2535, Dizeli Sh.2,301 na Mafuta ya taa ni Sh.2,272, Pwani lita ya petroli ni Sh.2,443, Dizeli Sh.2,226 mafuta ya taa Sh.2,192 huku Dodoma itakuwa petroli lita moja ni Sh.2,497, Dizeli Sh.2,320 na mafuta ya taa Sh.2,246,”amesema.Amebainisha kuwa kupunguzwa na kufutwa kwa baadhi ya tozo ambapo hatua hiyo imesaidia kutokuwa na ongezeko kubwa la bei za mafuta.

EWURA
error: Content is protected !!